Walimu wakuu wa shule za sekondari za umma walalamikia ukosefu wa fedha

  • | Citizen TV
    267 views

    Walimu wakuu wa shule za sekondari za umma humu nchini wanalalamikia changamoto zinazotokana na kucheleweshwa kwa fedha za ufadhili wa masomo kutoka kwa serikali kuu. Kufikia sasa, serikali imetoa shilingi elfu nne kwa kila mwanafunzi kinyume na matarajio ambapo kila mwanafunzi alistahili kupata shilingi elfu nane. Wizara ya elimu imetoa shilingi bilioni kumi na nne badala ya shilingi bilioni ishirini na nne zinazohitajika kwa muhula huu wa kwanza.