Mashirika ya KBC na Xinhua yadhamiria kushirikiana

  • | KBC Video
    10 views

    Shirika la utangazaji humu nchini-KBC na lile la habari la China, Xinhua yametia saini maafikiano yatakayofanikisha kutiwa saini kwa mkataba wa maelewano kuhusu ubia katika nyanja mbalimbali. Mkurugenzi mkuu wa KBC Agnes Kalekye amesema shirika hili linanuia kuimarisha sekta tatu muhimu ikiwemo kuboreshwa kwa vifaa vya kupeperusha matangazo, mafunzo ya kiteknolojia na ustawishaji wa mfumo wake wa kidijitali kupitia usaidizi wa shirika la habari la Xinhua. Kalekye aliyasema hayo alipopokea ujumbe kutoka shirika la Xinhua ukiongozwa na makamu wa rais wa shirika hilo duniani Yuan Bingzhong ambao walizuru jumba la utangazaji la KBC.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive