Nani ataibuka kuwa mwenyekiti wa AUC?

  • | BBC Swahili
    2,374 views
    Baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka saba kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), hatimaye Moussa Faki Mahamat sasa anaachia madaraka. Kuondoka kwake kunaacha pengo ambalo wagombea watatu wanachuana kuliziba. Walioidhinishwa kugombea wanatokea mashariki mwa Afrika ambao ni Raila Odinga wa Kenya, Moussa Ali Youssouf wa Djibouti, na Richard Randrimandrato wa Madagascar.