Familia zapokea mabaki ya miili ya walinda amani 14 waliouwawa DRC

  • | VOA Swahili
    4,718 views
    Mabaki ya miili ya walinda amani 14 wa Afrika Kusini waliouwawa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imerejeshwa nchini Alhamisi iliwasili katika Kituo cha Jeshi la Anga la Swartkop mjini Pretoria. Wanajeshi hao walifariki mwezi uliopita wakati wa mapigano kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23 ambapo walipelekwa huko kwa kazi maalum ya ulinzi wa amani. Majeneza ya wanajeshi hao yalifunikwa bendera za Afrika Kusini na yalibebwa na wanajeshi wa Jeshi la Anga kabla yakukabidhiwa kwa familia zilizo kuwa zikiomboleza vifo vyao. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa aliwaambia ndugu wenye huzuni wakati wa maombolezo hayo, “sisi kama raia wa Afrika Kusini tunawaona marehemu kuwa ni mashujaa wa taifa letu. "Majukumu yao huko DRC yalikuwa siyo tu kuimarisha utulivu. Ilikuwa ni kuhusu kujenga madaraja, kujenga amani, kuimarisha maelewano na kufungua njia mbalimbali za kuleta amani ya kudumu katika kanda yetu na bara letu,” - AP #drc #congo #m23 #reels #voa