Hifadhi haramu : Watoto-30 wanusuriwa

  • | KBC Video
    9 views

    Maafisa katika kaunti ya Kilifi wamenusuru watoto-30 kutoka kituo kimoja cha malezi ya watoto kinachosimamiwa na mume na mke kwa madai ya kutokuwa na kibali kinachohitajika. Wakiongozwa na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Malindi Irene Munyoki na afisa mkuu wa masuala ya watoto katika kaunti hiyo Sebastian Muteti, kundi hilo la maafisa lilielekea kwenye kituo hicho na kukifunga kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi. Wamiliki wa kituo hicho wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi. Watoto waliookolewa wamepatiwa hifadhi katika makai ya watoto yalioko Sabaki huku juhudi zikiendelea za kuwaunganisha na jamaa zao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive