Vijana waliouawa kwenye utata Majengo wafikia wawili

  • | Citizen TV
    2,396 views

    Idadi ya vijana waliouawa kufuatia vurumai lililozuka mtaani Majengo hapo jana imefikia wawili huku familia ya kijana mwingine ikidai jamaa yao aliuawa na polisi. Dennis Muthui anadaiwa kupigwa risasi wakati wa msako wa polisi eneo la Gikomba. Mashirika ya haki sasa yakitaka polisi kuwajibikia mauaji hayo, huku afisa aliyehusishwa na mauaji ya mvulana wa kwanza Ibrahim Ramadhan Chege akisimamishwa kazi.