Laura Seethal atoa kibao chake kipya Push 2 Start remix

  • | VOA Swahili
    30 views
    Mwanamuziki maarufu Laura Seethal al maarufu Tyla ametoa wiki hii, video ya wimbo wake mpya Push 2 Start remix akimshirikisha msanii nguli wa dancehall wa Jamaica Sean Paul. Wimbo huo mpya kutolewa unatokana na mfululizo wa albamu ndefu ya kwanza ya mwnamuziki huyu kinda mwenye umri wa miaka 23, iitwayi Tyla, ambayo ilitolewa Oktoba 2024. Mwanamuziki huyo mzaliwa wa Afrika Kusini alipata mafanikio wakati wimbo wake single amapiano Water ulipotamba kwenye TikTok. Wimbo huo ulishika nafasi ya saba kwenye Billboard Hot 100 ya Marekani na kuingia katika nyombo za juu 5 nchini Uingereza, na kumfanya kuwa msanii wa kike aliyeshika chati nyingi zaidi katika historia ya Afrika. Februari 19, ilitangazwa kuwa mwimbaji huyo wa Truth or Dare alikuwa msanii wa kwanza wa Kiafrika kupata kuangaliwa mara bilioni moja kwenye Spotify kwa wimbo wake uliotamba wa Water. Pia alishinda tuzo ya uzinduzi ya uchezaji bora wa muziki wa Kiafrika katika Grammys kwa wimbo huo. #mwanamuziki #lauraseethal #tyla #push2startremix #voa #voaswahili #burudani