Waziri Murkomen azindua magari maalum ya usalama

  • | KBC Video
    1,787 views

    Waziri wa usalama wa taifa Kipchuma Murkomen amesema ujangili katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi umepungua kwa asilimia sabini. Kipchumba amesema kuwa hali hii inatokana na kutumiwa kwa teknolojia ya kisasa kukabiliana na uhalifu. Kipchumba ambaye alizungumza alipozindua kundi la pili la magari maalum ya usalama katika makao makuu ya kitengo cha -GSU huko Ruaraka alisema kuwa magari hayo yatasaidia katika kupambana na wizi wa mifugo na ujambazi katika maeneo ya kaskazini mwa nchi na maeneo mengine ya mbali.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive