Serikali kupinga agizo la mahakama kuhusu ulipaji karo kupitia e-Citizen

  • | KBC Video
    20 views

    Wizara ya elimu iko mbioni kuandaa vikao vya ushirikishi wa umma ili kutimiza maagizo ya mahakama. Waziri wa elimu Julius Migos amesema wizara hiyo imekuwa ikiandaa ripoti ya kina tangu mwezi Oktoba mwaka 2023 ambayo itatoa mwongozo kuhusu hatua zitakazochukuliwa katika utekelezaji wa muundo mpya wa ulipaji karo katika vyuo vikuu vya humu nchini. Na haya yakijiri, katibu katika idara ya elimu ya msingi Profesa Julius Bitok amethibitisha kuwa wizara ya elimu imewasilisha rufaa mahakamani kupinga uamuzi wa mahakama kuu uliotaja ulipaji karo kupitia mfumo wa e-Citizen kuwa kinyume cha katiba.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive