Washukiwa saba wanaohusishwa na visa vya wizi wa magari katika barabara ya Mombasa-Nairobi wakamatwa

  • | Citizen TV
    549 views

    Watu saba ambao ni washukiwa wa visa mbalimbali vya uhalifu ikiwemo wizi wa magari katika barabara kuu ya Nairobi kuelekea Mombasa wanazuiliwa na polisi katika kituo cha Voi baada ya kukamatwa na maafisa wa usalama. Kamishna wa kaunti ya Taita Taveta Josephine Onunga amesema maafisa wa usalama wamewanasa washukiwa hao baada ya kupata ripoti za kijasusi kuhusu shughuli ambazo wamekuwa wakitekeleza ikiwemo utekaji nyara wa madereva wa malori ya masafa marefu.Onunga amesema maafisa wa usalama wameimarisha doria wakati huu wa sherehe za pasaka na kutoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wanapokua barabarani.Aidha amewahakikishia usalama wageni wote wanaozuru kaunti hiyo na hasa mbuga ya wanyamapori ya Tsavo.