Ouma Oluga achukua usukani kama Katibu wa Huduma za Afya katika Wizara ya Afya

  • | Citizen TV
    212 views

    Aliyekuwa katibu wa huduma za matibabu Harry Kimtai amempokeza rasmi ofisi Dkt. Ouma Oluga katika makao makuu ya wizara ya afya. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wazidi mpya wa ardhi aden duale, dkt. oluga ameapa kufanya kazi kwa ushirikiano na waziri mpya na makatibu ili kufanikisha huduma za matibabu. Dkt Oluga amesema kuwa japo wizara hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi, atafanya juhudi kuhakikisha kuwa huduma za afya zimeimarika na masahi ya wahudumu yameboreshwa.