Watu wawili wajeruhiwa kwenye makabiliano ya utata wa ardhi Mtwapa

  • | Citizen TV
    296 views

    Watu wawili wanauguza majeraja kufuatia makabiliano baina ya makundi hasimu yanayodai umiliki wa kipande cha ardhi huko ndonya mtwapa kaunti ya kilifi. Wawili hao wanadai kupigwa risasi na maafisa wa polisi. Hali hii imesababisha taharuki huku kundi moja likidai kuwa licha ya mzozo huo kuwa mahakamani bwenyenye mmoja akishirikiana na wanasiasa wanapanga njama ya kuwafurusha wakazi.