Wanawake eneo la Mukurwe-ini, Nyeri, wataka waume kuacha uraibu wa pombe

  • | Citizen TV
    226 views

    Ili kupunguza visa vya dhuluma za kinjisia vinavyoongezeka katika eneo bunge la mukurwe-ini kaunti ya nyeri , kina mama kutoka eneo hilo wamewarai vijana na wanaume kukoma matumizi ya dawa za kulevya na ubugiaji uliozidi wa vileo. Kwenye kikao cha kubuni mbinu za kuwapa mwanzo mpya waliodhulumiwa , Wanaharakati waliwaomba vijana kutokimbilia ndoa au kutafuta mbinu za mkato kupata pesa au mali ili kuimarisha maisha yao. Wanasema hali hiyo inasababisha ongezeko la dhulma. Kulingana na kamanda wa polisi Mukurwe-ini Beatrice Nyaga, visa 11 vya dhuluma vimeripotiwa mwaka huu, idadi ambayo anasema ni ya kutia wasiwasi.