Viongozi wa chama cha UPP waanza mikakati ya kujiimarisha

  • | Citizen TV
    676 views

    Viongozi wa chama cha United Progressive Party kutoka Kisii, Nyamira na Migori wameanzisha mchakato wa kuimarisha chama hicho huku wakimuidhinisha aliyekuwa waziri wa Usalama Dkt. Fred Matiangi kama mgombea kiti cha Urais katika uchaguzi ujao. Wakizungumza eneo la Bomachoge Chache katika mkutano uliwaoleta pamoja viongozi wa mashinani wa UPA kutoka kaunti hizo tatu, wanachama hao wanasema eneo la Gusii limehadaiwa kisiasa na hivyo sababu ya kuwa na mabadiliko ya mawimbi ya kisiasa.Aidha wamerai wakenya kuchukua vitambulisho vya kitaifa kwa wingi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027 ili washiriki uchaguzi.