Wakazi wa Ndabibi wataka hatimiliki za ardhi

  • | Citizen TV
    164 views

    Wakazi wa Ndabibi huko Naivasha wanamtaka rais William Ruto kutatua suala la utata wa ardhi na kuwasaidia kupata hatimiliki za ardhi wakisema kuwa walikabidhiwa barua za umiliki miaka 30 iliyopita. wakulima hao wanaopata elfu tano wameomba msamaha kwa kuvamia shamba la rais eneo hilo na kuharibu mali miezi kadhaa iliyopita. wakazi hao wanasema kuwa wamekuwa wakisubiri hatimiliki za ardhi tangu mwaka wa 1998. aidha wanasema kuwa eneo hilo limeachwa nyuma kimaendeleo na kumtaka rais kuzindua miradi ya barabara, hospitali na masoko.