Ford Kenya yasisitiza haitamezwa na UDA

  • | Citizen TV
    697 views

    Katibu mkuu wa chama cha Ford Kenya John Chikati amesema kuwa chama cha Ford Kenya hakitakubali kuvunjiliwa mbali na kuingia katika chama cha uda ila watafanya kazi pamoja hadi makubaliano yao yakamilike mwaka 2027 ambapo chama hicho kitakapoamua ni mrengo upi kitaungana nao. Chikati alizungumza alipowapokea wawakilishi wadi kutoka bonde la ufa waliogura vyama vyao na kujiunga na Ford Kenya.