Baraza la wazee wa jamii ya Abagusii latoa makataa kuhusu mgogoro wa uongozi Nyamira

  • | Citizen TV
    397 views

    Baraza la wazee wa jamii ya Abagusii limetoa makataa ya wiki mbili kwa wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Nyamira kuweka kando tofauti zao na kutafuta mwafaka.Wazee hao kutoka makundi ya Mwanyagetinge na BARAZA LA WAZEE WA Borabu wamesikitikia vurugu zinazoendelea katika bunge hilo, wakisema zimeathiri sana maendeleo na usimamizi wa mali ya umma katika kaunti ya Nyamira.