Je China imewezaje kwenda jino kwa jino na Marekani katika ushuru?

  • | BBC Swahili
    13,659 views
    Hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kuweka ushuru kwa bidhaa zinazotoka nchi mbalimbali ulimwenguni imezua taharuki kubwa ya kibiashara na uchumi nchini Marekani na kwingineko ulimwenguni. Tofauti na nchi nyingi, China imegoma kutii kirahisi matakwa ya Marekani, badala yake imelipiza kisasi katika kila hatua ambayo Marekani imeongeza ushuru. Mwandishi wa BBC Swammy Awami anaangazia katika video hii namna gani China imefanikiwa katika vita hii ya kiuchumi. 🎥: @eagansalla_gifted_sounds #bbcswahili #marekani #cjhina Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw