Jeshi la polisi Dar es Salaam latoa onyo kwa CHADEMA

  • | BBC Swahili
    19,748 views
    "Jeshi la polisi linatoa onyo kali kwa wale wote wanaopanga kutekeleza mpango huo kuwa watashughulikiwa vikali lakini kwa mujibu wa sheria" Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam limetoa onyo dhidi ya mpango wa Chadema kuhamasisha watu kukusanyika Mahakama ya Kisutu April 24 ili kumuunga mkono kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA Tundu Lissu atakapofikishwa Mahakamani hapo Onyo hilo limekuja baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche kusisitiza watu kujitokeza kwa wingi siku hiyo Kiongozi wa CHADEMA Tundu Lissu, alifunguliwa kesi kwa shutuma za uhaini baada ya kukamatwa mkoani Ruvuma alipokuwa kwenye kampeni ya kushinikiza mageuzi kwenye Tume ya Uchaguzi kabla ya uchaguzi wa mwezi Oktoba. - #bbcswahili #tanzania #uongozi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw