Mshukiwa wa mauaji ya mwanabodaboda Kabartonjo akamatwa

  • | Citizen TV
    723 views

    Polisi mjini Kabarnet wamefanikiwa kuupata mwili wa mhudumu wa bodaboda ambaye alikuwa ametoweka tangu Alhamisi, tarehe 17 Aprili. Hii ni baada ya mshukiwa kukamatwa katika mji wa Eldoret akiendesha pikipiki ya marehemu. Mshukiwa alikiri kumuua mwanaume huyo na kuwaongoza polisi hadi eneo la Kabartonjo, ambako alikuwa ameuficha mwili kwenye kichaka ndani ya bonde. Marehemu, Kevin Kibichii Togoch, anasemekana kuwa alipigiwa simu na mteja aliyekuwa ndani ya mji wa Kabarnet siku ya Alhamisi , simu ambayo inasadikika kuwa mtego kabla ya kutoweka.