Mwakilishi wa kike kaunti ya Nyamira atoa sare na mipira ya kandanda kwa vijana

  • | Citizen TV
    56 views

    Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Nyamira Jerusha Momanyi amewashauri vijana kujiunga na timu za michezo, ili kukuza talanta zao kama njia moja ya kujichumia riziki na kujiepusha na hulka mbaya katika jamii. Akizungumza kwenye hafla ya kutoa mipira na sare kwa timu za michezo kutoka eneo hilo, Momanyi amesema talanta zikikuzwa vyema zinaweza kuwaajiri vijana na kuwapa kipato kizuri. Aidha mwakilishi huyo wa kike alitoa mahema kwa vyama vya ushirika, huku akiwahimiza vijana na kina mama kujiunga kwenye vyama vya akiba na mikopo ili kupata ufadhili wa serikali.