Wahudumu wa afya kaunti ya Kisii watishia kuandamana

  • | Citizen TV
    154 views

    Viongozi wa miungano mbali mbali za kutetea haki za wahudumu wa afya katika kaunti ya Kisii wametishia kufanya maandamano dhidi ya waziri wa afya na usimamizi kutokana na madai ya kuhujumu utendakazi wao. Wakizungumza mjini Kisii wahudumu hao kutoka miungano ya wauguzi, maafisa wa kiliniki na Miungano mingine ya wahudumu wa afya wanasema kwamba iwapo mabadiliko hayatafinyika basi watakuwa na kibarua kigumu kutekeleza wajibu wao. Aidha wanadai kwamba kumekuwa na njama ya kuzuia viongozi wa miungano hiyo kukutana na gavana wa kaunti hiyo ili kuelezea masaibu yao.