Mwanaume awavamia mashemeji Kericho

  • | Citizen TV
    490 views

    Ndugu wawili kutoka kijiji cha Kunyak-Kapkwen katika eneobunge la Kipkelion Magharibi wanapokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kericho baada ya kushambuliwa na shemeji yao wakati wa kikao cha upatanisho wa wanandoa waliotengana. Inaripotiwa kuwa Mercy Chelangat mwenye umri wa miaka 27, mama wa watoto wawili, alishambuliwa nyumbani kwa wazazi wake na mumewe wa zamani Davis Kemei kwa kisu. Wanandoa hao walikuwa wametengana na walikuwa wamekutana na jamaa zao kutafuta suluhisho la amani. Kaka yake Mercy, Gilbert Kemboi, alijeruhiwa vibaya wakati alipojaribu kumlinda dada yake. Wote wawili wanatibiwa katika hospitali hiyo hiyo. Kemei naye alishambuliwa na umati wenye hasira na kupeleka hospitalini kwa matibabu.