Wakazi wataka wapewe ajira katika ujenzi wa uwanja wa ndege wa Karenga, kericho

  • | Citizen TV
    331 views

    Huku siku mbili tu zikisalia kabla ya uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kerenga kilomita nne kutoka mji wa Kericho, wakazi kutoka kaunti hiyo wamejitokeza na kutaka mamlaka ya viwanja vya ndege KAA pamoja na viongozi kuwashirikisha katika ujenzi huo . Kulingana nao, wanataka kupewa asilimia themanini ya kazi hiyo ya ujenzi. Vile vile vijana wameomba serikali kuweka ukurasa wa matangazo kwenye tovuti ili kuweka wazi mwanakandarasi na habari nyingine zinazohusiana na kandarasi hiyo.