Barabara ya eneo la Muslim wadi ya Musikoma huko Kanduyi haipitiki

  • | Citizen TV
    500 views

    Wakazi wa eneo la Muslim katika wadi ya Musikoma eneo bunge la kanduyi kaunti ya bungoma wamelalamikia hali mbovu ya barabara kuu ya muslim hadi kwa chifu wakisema inatatiza shughuli za usafiri. Wakazi hao wanadai kuwa msimu huu wa mvua barabara hiyo imeharibika na kusababisha ajali kila wakati . Wametoa wito kwa mwakilishi wadi wa eneo hilo george makari kujitokeza na kuwasilisha hoja hiyo katika bunge la kaunti ili kuhakikisha barabara hiyo inakarabatiwa.