Watu wawili wauawa kwenye uvamizi wa punde eneo la Loberer barabara ya Marigat-Chemolingot

  • | Citizen TV
    355 views

    Hali ya taharuki imetanda kaunti ya Baringo baada ya watu wawili kupigwa risasi eneo la Loberer kwenye barabara ya Marigat kuelekea Chemolingot. Waliouawa ni dereva wa lori na mfanyiabiashara waliokuwa wakielekea katika soko la mifugo la Nginyang. Wananchi waliokuwa na ghadhabu walikusanyika na kufunga barabara ya Marigat - Nakuru huku wakitaka serikali kuwajibikia usalama wao. viongozi wa baringo na wananchi wanalaumu walinda usalama kwa kuzembea kazini na kuitisha hongo barabarani badala ya kukabiliana na wahalifu. Hata hivyo Kamishna wa Baringo Sangolo Kutwa amesema kuwa polisi wamepata ushahidi wa kutosha na watawakamata wahusika wa mauaji hayo.