Skip to main content
Skip to main content

Samia Suluhu Hassan kuapishwa rasmi katika uwanja wa kijeshi Dodoma #tanzania #uchaguzi2025

  • | BBC Swahili
    34,154 views
    Duration: 41s
    Rais mteule wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuapishwa rasmi leo Jumatatu Novemba 3 Jijini Dodoma. Kupitia taarifa ya serikali kwenye runinga ya kitaifa ya TBC, Katibu mkuu kiongozi alisema hafla ya uapisho itafanyika katika uwanja wa kijeshi Dodoma. - Rais Samia alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29 kwa kujinyakulia asilimia 97.66 ya jumla ya kura zote zilizopigwa. Hata hivyo ushindi wake umepingwa na chama kikuu cha upinzani CHADEMA kikisema ni kejeli kwa demokrasia. - Aidha Chanzo cha kidiplomasia kiliiambia BBC kuwa kuna ushahidi wa kuaminika unaoonyesha kuwa angalau watu 500 wameuawa katika maandamano hayo. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Thabit Kombo, ameeleza kuwa serikali haiwezi kuthibitisha idadi hiyo rasmi. - - - #uchaguzi #uchaguzi2025 #tanzania #bbcswahili #siasa #foryou #chadema #maandamano #dodoma Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw