Skip to main content
Skip to main content

Vijana elfu-5 wapokea mafunzo kuhusu mpango wa NYOTA

  • | KBC Video
    49 views
    Duration: 1:32
    Takribani vijana 5,000 kutoka Kaunti ya Kakamega wamekamilisha mafunzo kuhusu ujasiriamali ya siku nne yaliyofadhiliwa na serikali ya kitaifa. Mafunzo hayo yaliandaliwa kabla ya vijana hao kukabidhiwa fedha kupitia mpango wa uwezeshaji wa NYOTA, ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Kenya na Benki ya Dunia. Vijana hao wameahidi kutumia fedha hizo kwa njia bora, ikiwemo kuanzisha na kuendeleza ,binu za kujikimu.Walisema mafunzo hayo yamekuwa yenye manufaa makubwa, kwani yamewapatia ujuzi muhimu wa ujasiriamali utakaowawezesha kusimamia vyema mtaji wa shilingi 50,000 kuanzisha au kukuza biashara zao. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #Kenya #News