Idadi ya watu waliopoteza makazi kufuatia ongezeko la maji kwenye Ziwa Naivasha imefikia 4,000 huku kukiwa na wasiwasi kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na mvua inayoendelea kunyesha. Tangu mwanzo wa mwaka huu, viwango vya maji katika Ziwa Naivasha vimekuwa vikiongezeka na hali imekuwa mbaya zaidi katika muda wa miezi mitatu iliyopita. Maji hayo yamefurika kwenye nyumba za makazi, vyoo, shule, makanisa na hata kituo kimoja cha polisi.Run vcr Aliyekuwa mkuu wa kitengo cha utoaji huduma za serikali, Peter Mbae, anasema mzozo wa kibinadamu unashuhudiwa katika eno hilo ambalo ni makao ya mamia ya wafanyakazi wa mashamba ya maua. Serikali ya kaunti ya Nakuru imejitolea kuwasafirisha wakazi ambao hawana fedha za kuwawezesha kuhamia mitaa iliyo karibu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News