Vijana kutoka vyuo mbalimbali wamezindua mpango wa kuhamasisha wenzao kujisajili kwa wingi kuwa wapiga kura, ili sauti zao zisikike wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Vijana hao wanasema wamesahauliwa kwa muda mrefu, na sasa ni wakati wao kutambuliwa katika uundaji wa serikali ijayo.Vuguvugu hilo lijulikanalo kama “Kiambu Youth Impact Circle (KYIC)” limewaleta pamoja vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 21.Wakizungumza mjini Kiambu wakati wa uzinduzi wa vuguvugu hilo, vijana hao waliwataka viongozi waliochaguliwa kuunga mkono mpango huo ili kuhakikisha wale waliotimiza umri wa kupata vitambulisho vya kitaifa wanavipata, ili washiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News