Serikali ya taifa imechukua hatua kusuluhisha tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji katika kaunti ya Kilifi kufuatia malalamishi ya wakazi na wawekezaji wa sekta ya utalii. Waziri wa maji, Eric Muga, aliongoza ujumbe wa maafisa wa serikali waliozuru kaunti hiyo ambao walibaini kwamba mtambo muhimu wa usambazaji maji umeharibika.Kaunti ya Kilifi imekuwa ikikumbwa na uhaba mkubwa wa maji huku kampuni za usambazaji maji za Kilifi Mariakani na ile ya Malindi zikishindwa kukidhi hitaji. Serikali imedhamiria kuweka mtambo unaotegemea kawi ya miale ya jua kusambaza maji katika eneo hilo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News