Skip to main content
Skip to main content

Kanisa Nandi latakiwa kuhamasisha jamii

  • | KBC Video
    39 views
    Duration: 1:16
    Shirika la Kitaifa la Udhibiti wa Pombe na Dawa za Kulevya (NACADA) limetoa wito kwa viongozi wa kidini kuchukua jukumu la moja kwa moja katika kushughulikia uraibu wa pombe na mihadarati katika Kaunti ya Nandi. Wito huo ulitolewa wakati wa kikao cha uhamasisho mjini Kapsabet ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya NACADA, Askofu Stephen Mairori, alisema taasisi za kidini zina jukumu muhimu katika kuratibu maadili ya kijamii na kusaidia familia zinazokabiliana na uraibu wa pombe. Askofu Mairori alisema viongozi wa kidini wanapaswa kuhamasisha watu ambao wamezama kwenye lindi la uraibu kuhusu huduma zinazopatikana za urekebishaji mienendo Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #Kenya #News