- 1,031 viewsDuration: 4:09Shughuli za kibinadamu katika mharara wa bonde la Kerio zimetambuliwa kuwa chanzo kikuu cha maporomoko ya ardhi yanayoendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Kufuatia hali hii serikali imehimizwa kuchukua hatua za dharura kuwahamisha wakazi wanaoishi katika maeneo yaliyo kwenye hatari ili kuepusha maafa zaidi. Wakati huo huo, wakazi wenye simanzi wa eneo la Chesongoch bado wana matumaini ya kuwapata jamaa wao waliopotea kufuatia maporomoko ya hivi majuzi. Idadi rasmi ya waliofariki imefikia watu 36, huku wengine 16 wakiwa bado hawajapatikana. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive