Wanaharakati wawili wa Kenya waliotoweka nchini Uganda na kushukiwa kuzuiliwa na serikali ya Uganda wameachiliwa huru. Bob Njagi na Nicholas Oyoo walipelekwa kwenye kwa Ubalozi wa Kenya, baada ya siku 38 tangu walipotoweka katika hali ya kutatanisha. Shughuli hii ilishirikishwa na maafisa wa taifa hilo na mashirika ya kibinadamu. Walipowasili kwenye kituo cha mpaka cha Busia, walipokelewa na Kamishna wa Kaunti ya Busia, Chaunga Mwachaunga.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive