Mahakama iliamua kwamba Kennedy Kiarie Kahochio, mshukiwa huyo anahusishwa na mauaji ya Sarah Wambui Mungai, aliyeaga dunia usiku wa tarehe sita mwezi Februari mwaka 2016, ana kesi ya kujibu. Kwingineko, changamoto ya kuongezeka kwa viwango vya maji kwenye ziwa Naivasha inaendelea kuathiri mitaa, mashamba na muundo msingi wa serikali ulio karibu. Waathiriwa wa hivi punde zaidi kuripotiwa ni taasisi ya mamilioni ya pesa ya utafiti na mafunzo kuhusu wanyama pori, kituo cha utafiti kuhusu maeneo chepechepe na kambi za viboko ambavyo vimesombwa na maji na hivyo kutatiza shughuli huku taasisi hiyo ikikadiria hasara za thamani ya mamilioni ya pesa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive