Watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa mwezi huu wa Novemba, kufuatia makabiliano kuhusu malisho na maji katika baadhi ya maeneo ya kaunti ya Marsabit. Makabiliano hayo yamechochewa na hali ya kiangazi inayoshamiri, jamii za wafugaji ziking'ang'ania maji na malisho. Naibu kamishna wa kaunti ya North Horr George Owuor amesema maafisa wa usalama wamepelekwa maeneo hayo kurejesha hali ya utulivu, huku ukame ukiendelea kukithiri. Ben Chumba ana taarifa kamili.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive