Vifo 924 vya kina mama wanaojifungua na elfu-20 vya watoto wachanga, vimeripotiwa nchini Kenya tangu mwezi Januari mwaka 2025. Sababu kuu ya vifo vya kina mama wajawazito imetambuliwa kuwa kutokwa na damu nyingi kupita kiasi, huku hali ya kukosa hewa ikichangia vifo vingi vya watoto wanaozaliwa. Baraza la magavana wakati uo huo, limeokosoa wizara ya afya na halmashauri ya Afya ya Jamii kwa madai ya kuzuia huduma za kina mama wajawazito katika zahanati, likisema hali hiyo imesababisha kupungua kwa idadi ya akina mama wanaotafuta msaada wakati wa kujifungua.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive