6,381 views
Duration: 8:19
Serikali ya Tanzania imesema haina nia ya kubana uhuru wa habari ama kunyanyasa wanahabari siku chache baada ya kusitisha leseni ya maudhui ya mtandaoni kwa jukwaa la JamiiForums. Akizungumza na BBC, Muasisi wa JamiiForums, Maxence Melo amesema wanalazimika kukubali uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kusitisha leseni yake ya maudhui kwa siku 90, japokuwa hawakubaliani nao. TCRA ilitangaza kusitisha leseni ya maudhui ya JamiiForums na kuzuia upatikanaji wake nchini kwa madai ya kukiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020 na marekebisho ya 2022.
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw