2,205 views
Duration: 3:49
Vyombo vya habari vya Israel vinaripoti kwamba maafisa wa ngazi za juu wa ulinzi wa Israel wanazidi kutilia shaka kama kweli viongozi wa Hamas waliuawa katika shambulio lililowalenga mjini Doha, mji mkuu wa Qatar jana Jumanne. Maafisa wa Qatar wamesema serikali imeelekeza timu ya kisheria kuchunguza uwezekano wa kumuwajibisha Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa kuvunja sheria za kimataifa. Rais wa Marekani Donald Trump, amesema hakufurahishwa kabisa na shambulio hilo dhidi ya mmoja wa washirika wa Marekani.
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw