Maandalizi ya mbio za Nyika za Chepsaita yamenoga

  • | Citizen TV
    100 views

    Maandalizi ya mbio za Nyika za Chepsaita katika kaunti ya Uasin Gishu yamepata kasi huku mbio hizo zikipangiwa kufanyika tarehe mbili mwezi Disemba. Mbio hizo zinalenga kukuza vipaji vya wanariadha na kuwapa vijana nafasi ya kushiriki michezo ili kujiendeleza na kuepukana na uhalifu na utumizi wa vileo na dawa za kulevya. Wanariadha wanatajika kimataifa wanatarajiwa kushiriki mbio hizo.