Henry Kissinger, aliyefariki Jumatano akiwa na umri wa miaka 100, alitengeneza sera ya binafsi ya mambo ya nje ya Marekani wakati wa uongozi wa Nixon na Ford, alihudumu katika wadhifa wa waziri wa mambo ya nje chini ya marais wote wawili na kukaribisha kumiminiwa sifa kwa mafanikio yake ya kidiplomasia na malumbano kwa kuanzisha maoni ya kisiasa ya ulimwengu.
Kifo cha kilitangazwa na kampuni yake ya ushauri na hakuna sababu iliyotolewa.
Alijulikana kwa kuwa msomi, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na mkimbizi maarufu aliyekuja Marekani, Kissinger alikuja kuwa ni mfano wa utamaduni, akihamasisha kuandikwa wasifu kadhaa, unaopendelewa na usiopendelewa, na kukashifiwa na mifano kama ya Monty Python.
Mwanafikra Mconservative alisaidia kuanzisha diplomasia kadhaa zilizofanikiwa, ikiwemo kufikia maelewano na China na kupunguza mivutano na Umoja wa Sovieti. Alipewa Tuzo ya Amani ya Nobel pamoja na Le Duc Tho wa Vietnam Kaskazini kwa juhudi zao za kuendesha mazungumzo yaliyomaliza Vita vya Vietnam. (VOA)
#HenryKissinger #Kissinger #US #China #Nixon #Vietnam