Droni za Iran zaisogelea karibu Manuari ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi

  • | VOA Swahili
    450 views
    Ndege isiyokuwa na rubani ya Iran iliruka takriban mita 1,370 karibu na manuari inayobeba ndege za kivita USS Dwight D. Elisenhower wakati ikirusha ndege zake katika eneo la majini la kimataifa Novemba 28, 2023, kulingana na taarifa iliyotolewa na Jeshi la Majini la Marekani. Naibu Mkuu wa Jeshi la Wanamaji Brad Cooper, kamanda wa Jeshi la Majini Kamandi ya Kati, alisema kuwa droni hiyo “ilikiuka tahadhari za kiusalama” kwa kutobakia zaidi ya maili 10 za mwendo wa baharini (kilomita 18.5) kutoka katika meli hiyo. Hakuna yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa na hakuna ndege iliyoharibiwa. Droni hiyo ilipuuza ilani kadhaa zilizotolewa lakini hatimaye iligeuza muelekeo wake. “Huu mwenendo usio salama, usiokuwa na weledi, na tabia ya kutowajibika inayofanywa na Iran inahatarisha uhai wa Wamarekani na mataifa washirika na lazima ukome mara moja,” alisema Cooper. (AP) #Iran #PersianGulf #voa #reels #igreels #videography