Jukumu la Kikanda la Misri Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Bara la Afrika .

  • | VOA Swahili
    121 views
    Katikati ya Mashariki ya Kati, Misri inasimama kama nguvu ya kikanda, ikiwa na jukumu muhimu katika migogoro na changamoto nyingi ambazo zinafafanua mienendo ya eneo hilo. Kuanzia kuhusika kwake katika mzozo wa Palestina na Israel hadi michango yake huko Yemen, Sudan, Libya, na hata kukabiliana na majanga ya asili kama tetemeko la ardhi la hivi karibuni huko Morocco. Wakati huo huo, eneo hilo bado liko kwenye njia panda kwa sababu ya mvutano unaoendelea Mashariki ya kati, kati ya Israel,palestine ,Yemen, Syria, Iraq na maeneo mengine ya migogoro, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka hivi karibuni nchini Sudan, pamoja na changamoto kuu zinazoletwa na uhusiano uliovunjika kati ya Iran, Israel, na nchi kadhaa za Ghuba ya Kiarabu - pamoja na athari za muda mrefu za maelewano dhaifu ya Irani na Saudi ambayo bado hayajatathminiwa kikamilifu.