Ukanda wa Gaza: Mapigano makali kati ya Israel na Hamas yaikumba miji mikubwa

  • | VOA Swahili
    283 views
    Mapigano makali yameendelea hivi leo Alhamisi katika miji mikubwa huko Ukanda wa Gaza wakati majeshi ya Israel na wanamgambo wa Hamas wanapambana na raia wa Palestina wakitafuta makazi salama yaliyopo ili kujiepusha na vita. Mapambano yalitokea huko Gaza City, sehemu za kaskazini ambako Israel imelilenga tangu kampeni yake ya awali ya kulitokomeza kundi la Hamas, pamoja na huko Khan Younis kusini mwa Gaza, sehemu ambayo imepanuliwa katika vita. Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema majeshi ya Israel wanakaribia eneo la ambalo Mkuu wa Hamas huko Gaza, Yahya Sinwar yuko na kwamba ni suala la muda mpaka wampate. Mapigano yamewasukuma raia mbali zaidi upande wa Kusini, na kuvuruga operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa na kuchochea kurejewa kwa maonyo ya kuongezeka kwa hali mbaya. Umoja wa Mataifa umesema maelfu ya watu wamewasili katika siku za karibuni huko Rafah, eneo ambalo liko karibu na mpaka wa kusini mwa Gaza. Rafah ni eneo pekee huko Gaza ambalo limepokea misaada michache ya kibinadamu wiki hii kutokana na kusambaa kwa ghasia upande wa kaskazini, UN imesema. Wakazi na waandishi wa habari wameripoti mashambulizi kadhaa ya anga ya Israel huko Rafah usiku kucha, huko wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas ikiripoti vifo 37. - VOA News #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #hospitali #Nasser #wagonjwa #madawa