| Washawishi mitandao wapewa mafunzo ya kuwamasisha vijana kuhusu umuhimu wa amani katika jamii

  • | VOA Swahili
    74 views
    Kupiga picha na video kuonyesha maeneo wanayotembelea, kazi wanazofanya ama maisha yao kwa ujumla imekuwa hulka ya vijana wengi ulimwenguni. Tabia hii huwafanya vijana kutumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii. Shirika la kijamii la Dream Achievers mjini Mombasa limetumia fursa hiyo kuwapa mafunzo vijana ambao wamekua mabalozi wa amani mitandaoni. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.