8,209 views
Duration: 57s
Mkesha wa maombolezi unatarajiwa kuandaliwa usiku wa leo huko Manchester Uingereza kufuatia maafa yaliyotokea kwenye hekalu la kiyahudi alhamisi.
Polisi nchini Uingereza wametangaza kwamba kuna watu wanaozuiliwa wakichunguzwa kwa kuhusika kwenye shambulizi hilo ambalo mhusika mkuu aliyetambuliwa kama Jihad Al-Shamie mwenye asili ya Syria aliuwawa jana na polisi.
Watu watatu waliojeruhiwa wanapokea matibabu hospitalini. Waziri Mkuu wa Uingerza Kier Starmer aliyeongoza kikao maalum cha usalama hapo jana amelitaja shambulizi hilo kama tukio la kigaidi na kuitaka taifa hilo kulaani dhuluma za aina hiyo ambazo huenda zikatenganisha jamii. Polisi wamesema kwamba uchunguzi unaendelea. @RoncliffeOdit ana angazia taarifa hiyo na mengine mengi kwenye Dira ya Dunia Tv mubashara saa tatu usiku kupitia ukurasa wa YouTube wa BBC Swahili.
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw