- 15,722 viewsDuration: 5:05Familia ya aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole imewasilisha ombi mahakamani kumtaka kufikishwa mahakamani kufuatia kutoweka kwake. Wakili wake Peter Kibatala ameiomba mahakama kuishinikiza serikali ya Tanzania kupitia idara husika za usalama nchini humo kumuwasilisha mahakamani huku familia yake ikieleza wasiwasi wao kuhusu alipo mpendwa wao. Humphrey Polepole anaripotiwa kuchukuliwa kutoka nyumbani kwake mtaa wa Ununio wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam. #dirayaduniatv