Oparanya atishia kujiondoa mawazo yake yasipotekelezwa

  • | KBC Video
    440 views

    Waziri wa vyama vya ushirika na ustawi wa biashara ndogo ndogo na zile za kadri Wycliffe Oparanya ameonya kwamba atajiondoa serikalini iwapo utawala wa Kenya kwanza hautatekeleza mawazo yake. Akiwahutubia waumini katika kanisa la Church of God mtaani South B, Oparanya hata hivyo alisema kuwa ataongoza wizara hiyo kuunga mkono wafanyabiashara ndogo ndogo na zile za kadri ili kubuni nafasi zaidi za ajira hasa kwa vijana. Viongozi wa ODM akiwemo naibu kiongozi wa chama Godfrey Osotsi walisema kuwa chama cha ODM hakitalaumiwa iwapo serikali haitatimiza matarajio ya wananchi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive