Wiki ya kuangazia madhara ya madini ya risasi yaanza

  • | KBC Video
    66 views

    Wizara ya afya itarekebisha sheria kuhusu kemikali zinazoharibu mazingira yakiwemo madini ya risasi huku takwimu za kusikitisha zikionyesha kwamba watoto laki sita nchini huwa na matatizo ya kimasomo kutokana na sumu ya madini ya risasi. Haya yalibainishwa huku Kenya ikiungana na ulimwengu kwa makala ya 12 ya juma la kimataifa la kuzuia sumu ya madini ya risasi. Takwimu za kimataifa za shirika la USAID zinaonyesha kwamba mtoto mmoja kati ya wawili hukabiliwa na hatari ya kuathirika kutokana na sumu ya madini ya risasi huku vifo milioni moja vikinakiliwa kila mwaka. Mwanahabari wetu Kasichana Masha anatuarifu zaidi kuhusu tishio la sumu ya madini ya risasi linaloibua wasiwasi wa kiafya na kimazingira.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive