Mkenya atangazwa mshindi Tuzo ya Komla Dumor ya BBC News 2024

  • | BBC Swahili
    482 views
    Rukia ni mwandishi wa habari wa Nation Media Group na amejipatia umaarufu mkubwa kwenye TikTok kupitia maudhui yake yanayohusiana na maisha ya mwandishi wa habari. Katika sehemu ya tuzo hiyo, Rukia atatumia miezi mitatu akifanya kazi BBC News katika upande wa televisheni, redio na mtandaoni huko London, ambapo atapata ujuzi muhimu na fursa nyingine. Tuzo ya Komla Dumor ilianzishwa mwaka 2015 kwa heshima ya mtangazaji wa Ghana na mwandishi wa habari wa BBC, Komla Dumor, anayejulikana kwa ustadi wake wa uandishi wa habari na kujitolea kwake kuwasilisha ripoti za Afrika kwa uhalisia. #bbcswahili #bbckomladumor #bbckomladumoraward Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw